Kamanda Sirro amesema
bado wanamshikilia mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji pamoja Askofu wa
kanisa la Ufunuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa tuhuma za kujihusisha na
biashara ya madawa ya kulevya na upelelezi dhidi yao bado haujakamilika.
Watuhumiwa hao wawili waliripoti kituoni hapo jana mchana na
siyo leo kama walivyoagizwa na RC Paul Makonda.
Kamanda Sirro amesema atatoa taarifa Jumatatu kueleza nini
kinaendelea kuhusu watuhumiwa hao.
Mpaka wakati anazungumza na waandishi wa habari kamanda huyo
alisema walioripoti kituoni hapo ni watuhumiwa 4 kati ya 65 .
Walioshuhudiwa na waandishi wa habari wakiripoti kituoni
hapo ni Iddi Azzan, Hussain Pamba Kali pamoja na bosi Sea Cliff.
No comments:
Post a Comment