Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema atamuagiza Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kuchunguza ukusanyaji mapato ya Shirika
la Ndege Tanzania(ATCL)
Ameyasema hayo jana
alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam kwa lengo
la kujionea mwenendo wa uendeshaji wake.
“Nitamuagiza CAG aje
aangalie mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya shirika hili kuanzia mwaka jana
lilipoanza kufanya kazi hadi sasa,” alisema Majaliwa.
Alisema kuwa Serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa
tena, hivyo amewataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio kwa
manufaa ya Taifa.
Pia aliwataka waache kukusanya mapato kwa kutumia risiti za kuandika kwa mkono na badala yake
waanze kutumia mfumo wa kieletroniki ili kuzuia upotevu wa mapato hayo.
Katika hatua nyinginre, Waziri Mkuu amemtaka Kaimu
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Witness Mbaga ajiridhishe na fedha
zinazokusanywa katika eneo la mizigo kama ziko sahihi, lengo ni kudhibiti
upotevu wa mapato.
Aidha, Waziri Mkuu
aliwataka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingatia ratiba ya njia na
muda wa safari ili wasipoteze wateja.
No comments:
Post a Comment