Pep Gurdiola anaendelea kuonekana wakawaida akiwa
Uingereza.Tofauti na alipokuwa Hispania na baadae Ujerumani Pep haonekani kuwa
na makali yaleyale ya alikotoka.Man City wamekuwa hawaeleweki msimu huu na
kidogo ujio wa bwanamdogo Gabriel Jesus amewaokoa wikiendi iliyopita.
Sasa baada ya Gurdiola kuona hali inazidi kuwa mbaya Man
City ameamua kufanya maamuzi magumu.Taarifa zinasema Pep anataka kupunguza
wachezaji 12 katika kikosi chake na kuleta wapya.Pep Gurdiola anaona wachezaji
wengi wa City hawaendani na mfumo wake hivyo inabidi aondoke.
Inajulikana kwamba mshambuliaji wa Man City Kun Aguero
ameanza kupoteza namba kwa Jesus.Katika mechi mbili mfululizo zilizopita Aguero
alikaa jukwaani akimuangalia Jesus akifunga tu.Sio rahisi kwa mshambuliaji
aliye na kiwango cha Aguero kukubali kusota jukwaani,anaweza kuwa mmoja ya
wachezaji wanaoondoka.
Lakini Bravo pia golikipa wao pamoja na Yaya Toure japo
anacheza lakini hana uhusiano mzuri sana na Pep na hii inaweza kumfanya
aondoke.Gurdiola amekuwa akiamini sana vijana wadogo hasa katika timu ya City
kwani unaweza kuona Sane,Sterling na Jesus walivyoweza kuaminika na kweli
kuanza kuleta matokeo.Hii inamaanisha wachezaji wenye umri mkubwa wanaweza
kufunguliwa mlango wa kutokea katika dirisha lijalo la usajili.
Wakati Gurdiola akipunguza watu lakini tayari ametenga £
200m kwa ajili ya usajili.Na inafahamika Gurdiola anataka kusajili mabeki
wawili,kiungo mmoja na striker.Mabeki wamekuwa tatizo kwake kwani beki wao
Stones waliyemsajili kutoka Everton siku za usoni amekuwa akiigharimu sana timu
kwa makosa yake na pia muunganiko wake na Otamendi umekuwa hauelewani.Lazima
Gurdiola atatafuta mtu wa kuja kukaa na Stones kama pacha au kujenga upya
kabisa eneo la beki.
Ikey Gundogan nae alikuja City akiwa na majeruhi ambayo bado
yanamuandama na kushindwa kucheza.Inaonekna Gurdiola anampenda Gundogan tofauti
na viungo wengine aliowakuta City.Lakini ameshindwa kabisa kumtumia na sasa ni
dhahiri Gurdiola atatafuta kiungo mwingine ambae anafanana kiuchezaji na Ikey
Gundogan.
Katika upande wa ushambuliaji imeripotiwa mara kadhaa City
walijaribu kumuunganisha Gurdiola na mchezaji wake wa zamani Lioneil Messi.City
bado wanahusishwa na usajili huo ambao unaweza kuvunja rekodi ya dunia na hata
kama sio Messi bado Gurdiola anahitaji mtu wa kuwapa changamoto washambuliaji
wake wa sasa.
No comments:
Post a Comment