
KUNA mambo mengi yamekuwa yakitokea duniani, yanashangaza na
wakati mwingine mtu kujiuliza kwamba inawezekanaje jambo hilo kutokea? Tangu
dunia ilipoumbwa, kuna mambo mengi yalitokea kuanzia karne ya 18 mpaka karne
hii ya 21.
Yapo yaliyotokea kwa makusudi lakini pia yapo yaliyotokea
kwa bahati mbaya kabisa ambayo kwa kifupi tungesema Mungu alitaka hayo yatokee
ili iwe fundisho kwa watu wanaoshuhudia au akusikia. Haya hapa ni baadhi ya
mambo matukio matano ambayo yaliishangaza dunia.

Kulipuliwa kwa Miji ya Nagasaki na Hiroshima.
Ni mwaka 1945 ambapo Vita vya Pili vya Dunia (WWII) vilikuwa
vimepamba moto. Mataifa mengi yakaungana kwa ajili ya kushambuliana huku
Ujerumani iliyokuwa chini ya Adolf Hitler ikiwa imeungana na Italia, Japan na
nchi nyingine.
Zilikuwa zikipambana na kundi jingine lililokuwa na nchi
kama Uingereza, Ufaransa na nchi nyinginezo. Vilikuwa vi vita vikali, walipambana
kwa nguvu kubwa na ndiyo ilikuwa vita pekee ambayo Marekani aliitumia
kutengeneza nchi yake.
Wakati wenzake wakiwa kwenye vita, kazi yake ilikuwa ni
kuitengeneza nchi, alikuwa akiwauzia Waingereza na wenzao nguo, chakula na
silaha. Vita viliendelea mpaka pale ndege ya Marekani ilipolipuliwa na Japan
kitu kilicholeta mtafaruku mkubwa kwamba kwa nini Japan ailipue ndege hiyo,
huku japan akiinuka na kusema kwamba kwa nini Marekani awauzie Waingereza
silaha na chakula na wakati yeye hakuhusika kwenye vita hivyo?
Japan hakubaki kimya, alidhamiria kumuingiza Marekani katika
ugomvi huu kwa kushambulia miji kadhaa nchini Marekani. Hapo ndipo rais wa
Marekani Harry S. Truman alipouliza kuhusu silaha walizokuwanazo na kuambiwa
kwamba walikuwa na mabomu mawili ya nyuklia na yalikuwa hatari sana. Akaagiza
hayohayo yaende kushambulia Miji ya Nagasaki na Hiroshima nchini Japan.
Kilichotokea huko, hakika Wajapan hawatokisahau na kuanzia siku hiyo,
hawakutaka tena vita.

Kifo cha John F Kennedy
Ni mwaka 1963 ambapo Rais wa 35 wa Marekani, John F Kennedy
alikuwa kwenye msafara wake uliokwenda kutembelea Jiji la Dallas, Texas. Wakati
akiwa na mkewe kwenye gari lililokuwa wazi kwa juu, jamaa mmoja aliyeitwa Lee
Harvey Oswald (Mdunguaji) alikaa kwenye ghorofa akiwa na bunduki yake kisha
kumpiga risasi Kennedy kwenye kichogo na kufariki hapohapo.
Huyo alikuwa rais wa mwisho wa Marekani kuuawa na tangu siku
hiyo wakatangaza kwamba hakutokuwa na rais wao yeyote atakayeuawa, hivyo
wakaongeza ulinzi maradufu. Kwa muuaji Oswald, alikamatwa ila kabla ya kupewa
hukumu yake, akauawa gerezani kwa kitu kilichohusishwa kwa kupoteza ushahidi.

Mwanadamu wa kwanza kufika mwezini
Hebu usiku toka ndani na kwenda nje, kisha angalia angani,
bila shaka utauona mwezi, si upo mbali, basi nataka nikwambie kwamba katika
matukio yaliyowahi kuishangaza dunia ni kitendo cha binadamu wa kwanza kufika
huko.
Ilikuwa mwaka 1968, Mmarekani, Neil Armstrong alipoamua
kufika mwezini kwa kutumia chombo kilichoitwa Apollo 11. Ilionekana kama
kushindikana lakini mwisho wa siku mtu huyo alifika huko na kukaa kwa saa 21.
Alipofika, kwanza hakutoka nje ya chombo hicho kwa muda wa saa sita, alibaki
ndani huku akijiuliza kama alitakiwa kutoka au la, ila mwisho wa siku akatoka.
Dunia iliweka historia, kila mtu akamuona Armstrong kuwa
shujaa mkubwa ambaye alifanya kile ambacho binadamu wengine waliona kwamba
isingewezekana hata kidogo. Baada yake, kulikuwa na watu wengine waliokwenda.
Kwa sasa, watu wanafikiria kwenye sayari ya Mars

Kuzama kwa meli ya Titanic
Ilikuwa mwaka 1912 siku ambayo meli ya Titanic ilitakiwa
kuanza safari yake kutoka Southampton nchini Uingereza na kwenda New York
nchini MArekani.
Ilikuwa meli kubwa na watu walioitengeneza walijivunia kwa
kusema kwamba isingeweza kuzama kwani ilikuwa imara sana, tena sana.
Meli hii ilibeba abiria 2224 na ilipozama siku nne baadaye
iliua abiria 1635. Mara baada ya taarifa kutangazwa, watu wengi walishtuka
kwani waliamini kwamba kwa ukubwa wa meli hiyo, uimara wake usingeweza kuzama
hata mara moja na waliamini kwamba ingefanya safari ndefu kuliko meli zote.
Meli hiyo ilizama baada ya kugonga mwamba wa barafu katika
Bahari ya Atlantiki inayotenganisha Marekani na Bara la Ulaya.
Kwa stori zote kali, Tu-follow
Facebook @BoazMwakasegePage
No comments:
Post a Comment