Kauli ya leo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Paul Makonda kwamba ana
uwezo wa kumhamisha mtu yeyote kutoka kwenye Mkoa wake ni mfano mwingine wa
aina ya wanasiasa waliopewa madaraka na Rais Magufuli ambayo hata hawayaelewi
na, kwa sababu hiyo, hata wao wenyewe hawajielewi.
Nafasi ya Wakuu wa Mikoa imetambuliwa na ibara ya 61 ya
Katiba yetu. Ibara ya 61(4) inafafanua kwamba kila Mkuu wa Mkoa atatekeleza
kazi na majukumu yaliyofafanuliwa na, au chini ya, sheria yoyote iliyotungwa na
Bunge.
Sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili ya kufafanua kazi na
majukumu ya Wakuu wa Mikoa ni Sheria ya Tawala za Mikoa ya 1997.
Sheria hiyo ndiyo iliyowapa Wakuu wa Mikoa na Wilaya mamlaka
ya kipolisi, yaani mamlaka ya kukamata watu wanaosadikiwa kufanya makosa ya
jinai mahali ambapo hakuna askari polisi.
Mamlaka haya ni madogo sana tofauti na Wakuu wa Mikoa au
Wilaya wa aina ya Makonda wanavyoamini au kuaminishwa.
Kwanza, ni mamlaka ya nyongeza (supplementary powers) tu kwa
mamlaka ya Jeshi la Polisi ambalo ndilo lenye mamlaka hasa ya kukamata
wahalifu.
Hii ina maana kwamba Mkuu wa Mkoa au Wilaya hawezi kutumia
mamlaka ya kipolisi pale ambapo tayari kuna askari polisi. Polisi wanatakiwa
wafanye kazi yao bila kuamriwa na Mkuu wa Mkoa au Wilaya.
Pili, mamlaka ya kipolisi yamewekewa masharti ya muda,
yaani, mtu aliyekamatwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya anatakiwa apelekwe mahakamani
au aachiliwe huru ndani ya muda wa masaa 48.
Tatu, Mkuu wa Mkoa au Wilaya aliyetoa amri ya kukamata mtu
chini ya mamlaka yake ya kipolisi, anatakiwa - haraka iwezekanavyo - kupeleka
taarifa ya maandishi kwa hakimu juu ya kukamatwa kwa mtu huyo na sababu zake.
Sheria imeweka wazi kwamba Mkuu wa Mkoa au Wilaya
asiyetekeleza masharti haya hataruhusiwa kumkamata mtu huyo kwa kosa hilo hilo
na anaweza kushtakiwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka yake.
Hakuna mahali popote katika Sheria ya Tawala za Mikoa ambako
Mkuu wa Mkoa au Wilaya amepewa mamlaka ya kumwondoa mtu yeyote kwenye Mkoa au
Wilaya yake.
Mamlaka ya kuondoa watu kwenye maeneo yao, yaani
deportation, yalikuwa sehemu ya mamlaka ya Rais kwa mujibu wa Sheria ya Kuondoa
Watu (Deportation Ordinance).
Sheria hii ya kikoloni ilitangazwa kuwa kinyume na Katiba,
na kwa hiyo batili, na Jaji James Mwalusanya wa Mahakama Kuu katika kesi
maarufu ya Chumchua Marwa na Wenzake ya mwaka 1987.
Ni wazi Mkuu wa Mkoa wa aina ya Paul Makonda hawezi kufahamu
mambo makubwa kama haya. Kwake yeye na kwa Wakuu wa Mikoa au Wilaya wa aina
yake, kuwa Mkuu wa Wilaya au Mkoa ni sawa na kuwa Rais wa Mkoa au Wilaya
aliyokabidhiwa.
Wakuu wa aina hii wanahitaji kuelimishwa kwamba wao hawana
mamlaka ya kifalme aliyo nayo Magufuli.
Na namna bora kabisa ya kuwaelimisha ni kuwashtaki kwa madai
mahakamani pale wanapoenda nje ya masharti ya madaraka yao. Tutaanza na Paul
Makonda.

Kauli ya leo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Paul Makonda kwamba ana
uwezo wa kumhamisha mtu yeyote kutoka kwenye Mkoa wake ni mfano mwingine wa
aina ya wanasiasa waliopewa madaraka na Rais Magufuli ambayo hata hawayaelewi
na, kwa sababu hiyo, hata wao wenyewe hawajielewi.
Nafasi ya Wakuu wa Mikoa imetambuliwa na ibara ya 61 ya
Katiba yetu. Ibara ya 61(4) inafafanua kwamba kila Mkuu wa Mkoa atatekeleza
kazi na majukumu yaliyofafanuliwa na, au chini ya, sheria yoyote iliyotungwa na
Bunge.
Sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili ya kufafanua kazi na
majukumu ya Wakuu wa Mikoa ni Sheria ya Tawala za Mikoa ya 1997.
Sheria hiyo ndiyo iliyowapa Wakuu wa Mikoa na Wilaya mamlaka
ya kipolisi, yaani mamlaka ya kukamata watu wanaosadikiwa kufanya makosa ya
jinai mahali ambapo hakuna askari polisi.
Mamlaka haya ni madogo sana tofauti na Wakuu wa Mikoa au
Wilaya wa aina ya Makonda wanavyoamini au kuaminishwa.
Kwanza, ni mamlaka ya nyongeza (supplementary powers) tu kwa
mamlaka ya Jeshi la Polisi ambalo ndilo lenye mamlaka hasa ya kukamata
wahalifu.
Hii ina maana kwamba Mkuu wa Mkoa au Wilaya hawezi kutumia
mamlaka ya kipolisi pale ambapo tayari kuna askari polisi. Polisi wanatakiwa
wafanye kazi yao bila kuamriwa na Mkuu wa Mkoa au Wilaya.
Pili, mamlaka ya kipolisi yamewekewa masharti ya muda,
yaani, mtu aliyekamatwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya anatakiwa apelekwe
mahakamani au aachiliwe huru ndani ya muda wa masaa 48.
Tatu, Mkuu wa Mkoa au Wilaya aliyetoa amri ya kukamata mtu
chini ya mamlaka yake ya kipolisi, anatakiwa - haraka iwezekanavyo - kupeleka
taarifa ya maandishi kwa hakimu juu ya kukamatwa kwa mtu huyo na sababu zake.
Sheria imeweka wazi kwamba Mkuu wa Mkoa au Wilaya
asiyetekeleza masharti haya hataruhusiwa kumkamata mtu huyo kwa kosa hilo hilo
na anaweza kushtakiwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka yake.
Hakuna mahali popote katika Sheria ya Tawala za Mikoa ambako
Mkuu wa Mkoa au Wilaya amepewa mamlaka ya kumwondoa mtu yeyote kwenye Mkoa au
Wilaya yake.
Mamlaka ya kuondoa watu kwenye maeneo yao, yaani
deportation, yalikuwa sehemu ya mamlaka ya Rais kwa mujibu wa Sheria ya Kuondoa
Watu (Deportation Ordinance).
Sheria hii ya kikoloni ilitangazwa kuwa kinyume na Katiba,
na kwa hiyo batili, na Jaji James Mwalusanya wa Mahakama Kuu katika kesi maarufu
ya Chumchua Marwa na Wenzake ya mwaka 1987.
Ni wazi Mkuu wa Mkoa wa aina ya Paul Makonda hawezi kufahamu
mambo makubwa kama haya. Kwake yeye na kwa Wakuu wa Mikoa au Wilaya wa aina
yake, kuwa Mkuu wa Wilaya au Mkoa ni sawa na kuwa Rais wa Mkoa au Wilaya
aliyokabidhiwa.
Wakuu wa aina hii wanahitaji kuelimishwa kwamba wao hawana
mamlaka ya kifalme aliyo nayo Magufuli.
Na namna bora kabisa ya kuwaelimisha ni kuwashtaki kwa madai
mahakamani pale wanapoenda nje ya masharti ya madaraka yao. Tutaanza na Paul
Makonda.
No comments:
Post a Comment