
Jumuiya ya Wenye magari ya kubeba mchanga visiwani Zanzibar
imesema muda waliopangiwa na Serikali wa kuingia na kutoka katika mashimo ya
kuchimbia mchanga utasababisha madereva wengi kupoteza nafasi zao za ajira
kutokana na hasara inayopatikana ikiwemo kufanya kazi mara moja kwa siku pamoja
na mzigo mkubwa wa kodi unaowakabili.
Akizungumza na waandishi wa habari katika shimo la kuchimbia
mchanga liliopo eneo la Bumbwini, Wilaya ya Magharib B, Mwenyekiti wa Jumuiya
hiyo Msabah Hassan Silima amesema hivi sasa eneo hilo linakabiliwa na
msongamano mkubwa wa magari kutokana na utaratibu uliowekwa wa kuingia shimoni
kuanzia saa moja za asubuhi na kutoka saa kumi za jioni.
Channel Ten imeshuhudia msongamano mkubwa wa malori
yanayobeba mchanga yanayoingia na kutoka katika shimo hilo, ambalo limepangiwa
utaratibu wa kutumika kwa siku tano kwa wiki huku magari hayo yakizuiliwa
kuondoka au kunyimwa vibali pale inapopindukia muda uliopangwa na Serikali.
Baadhi ya Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maghrib B,
wamekiri kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika eneo hilo, na kutoa ushauri
kwa viongozi wa ngazi za juu wa Serikali kuwashirikisha wadau wote wa sekta
hiyo kabla ya kufanya mabadiliko yoyote ya sheria na taratibu za uchimbaji wa
mchanga.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema hivi sasa kuna
eneo dogo lililoba
No comments:
Post a Comment