Mkalimani katika mbuga ya wanyama pori nchini Tanzania
amekamatwa baada ya kutafsiri visivyo matamshi ya mtalii mmoja kuhusu nchi na
watu wake.
Kwenye video iliyosambazwa kwa wingi, mkalimani huyo anasema
kuwa mtalii huyo anataka watu wa Tanzania waache kulalamika kwa sababu ya njaa
Ukweli ni kwamba mwananke huyo anasema kuwa wata wa Tanzania
ni wazuri kupindukia.
Alikamatwa siku ya Alhamisi kwa agizo la waziri wa utalii.
Mkalimani huyo ambaye hakutajwa jina ni kutoka mbuga ya
Serengeti iliyo kaskazini magharibi mwa nchi.
Video hiyo iliyochapishwa na gazeti la Kenya, mtalii
anasema:
"Hi. Ziara yangu nchini Tanzania imekuwa nzuri. watu ni
wazui na wenye urafiki. Salamu kwa kawaida ni Jambo, nina furaha kuwa hapa,
Ardhi ni nzuri."
Mkalimani anatafsiri hivi:
"Anasema watanzania mnalia sana njaa, kila siku mnalia
nja wakati mna maua nyumbani, si mchemshe maua mnywe, anasema si vizuri kulia
njaa."
Mtalii
"Aina nyingi ya wanyama na watu unaona ni wazuri,
kinyume na sehemu zingine. Ni nzuri."
Mkalimani
"Anasema mnamuomba rais wenu awapikie chakula, kwani
rais wenu ni mpishi, angahikeni mfanye kazi,chemsheni hata nguo mnywe."
Mtalii
"Ni kitu mabacho utakikumbuka katika maisha yako yote.
Ni nzuri na ni ya kupendeza."
Mkalimani
"Anasema mhangaikeni pembezoni za nchi, muache rais
hawezi kutoka Ikulu akuje kuwapikia chakula, hivyo mjipikie wenyewe."
No comments:
Post a Comment