
Ugomvi baina ya wapenzi katika mahusiano ni kitu cha kawaida
kutokana na watu hao wawili kutoka katika malezi na mazingira tofauti ya ukuaji
toka wakiwa wadogo hadi watu wazima.
Wawili hao wanapoaanza kujenga mahusiano na kukaa pamoja
kama familia,kuna vitu kadhaa ambavyo kila mmoja wao huvitazama tofauti na
hivyo kuleta migongano. Migongano ambayo inaweza ikarekebishika kama wenza hao
watamua kuifanyia kazi na kuelewana.
Kuna vitu vingi ambavyo husababisha ugomvi na migongano
ndani ya mahusiano ya mke na mme na hapa tunaeleza sababu kuu ambazo kwa
kawaida hutokea karibu katika kila mahususiano
1. Wivu Na Kukosa Kujiamini
Wivu unatokana na jinsi ambavyo mpenzi mmoja anavyohusiana
na watu wengine wa jinsia tofauti. Inaweza ikawa marafiki,wafanyakazi wenza au
wapenzi wa zamani. Vyovyote vile itakavyokuwa ni kwamba wivu unasababisha
ugomvi katika mahusiano mengi.
Kunatakiwa kuweka mipaka ya kutosha na iliyo wazi ili
kujenga uaminifu kwa mpenzi wako na kumpa kujiamini. Mpenzi ambaye hajiamini ni
tatizo kubwa kwani uwezekano wa kuanzisha ugomvi ni mkubwa.Hivyo ni vizuri
ukamjengea mweza wako katika mapenzi kujiamini kwa kuwa mwaminifu.
Uaminifu ni kitu kimoja kikubwa sana katika mapenzi. Kama
mwenza wako akikuamini hakutakuwa na wivu wa kupita kiasi na pia atakuwa
anajiamini kuwa yeye peke yake ndio chaguo lako na hakuna mwingine.
2. Mawasiliano Finyu
Mawasiliano yanapovunjika katika mahusiano ugomvi ni kitu
cha kawaida kutokea.
Mawasiliano ya kawaida kati ya wapenzi husaidia sana kutoa
wasiwasi wa nyendo za mwenza wako. Huleta amani na kujenga uaminifu kwa mpenzi
kwako.
Kuzungumza juu ya mipango yako ya mendeleo kama ujenzi au
biashara ni vitu ambavyo ni muhimu sana kuvifanya vinginevyo utajenga wasiwasi
kwa mweza wako na itasababisha ugomvi wa mara kwa mara.
Kuwa muwazi kwa mipango ya maendeleo binafsi,ya familia yako
na ndugu.
Utafiti unaonyesha kuwa wapenzi wanaoongea na kusikilizana
mara kwa mara hawagombani mara nyingi kama wale wasio na mawasiliano ya
kutosha.
3. Masuala Ya Fedha
Japokuwa fedha si msingi wa mapenzi,lakini ni kitu ambacho
kinahitajika sana katika maisha ya kila siku ya kila mtu na ya familia. Na
kimekuwa ni mojawapo ya vitu ambavyo wapenzi katika mahusiano au ndoa hugombana
sana juu yake.
Mwenza mmoja anapokuwa mtumiaji mbaya wa fedha na mwingine
siyo,huibua malalamiko na ugomvi. Baadhi ya wapenzi hasa wanawake hawataki
kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mahitaji ya msingi ya nyumbani na badala
yake kuwaachia mzigo mkubwa wanaume.
Hili linaibua malalamiko mengi kwa baadhi ya wanaume,na
wakati ungine toka kwa wanawake. Matumizi makubwa ya fedha kwaajili ya pombe na
sharehe nyingine kwa wanaume na baadhi ya wanawake kumekuwa mojawapo ya sababu
za ugomvi juu ya fedha katika mahusiano.
Ni muhimu kwa wenza wawili kupanga jinsi ambavyo fedha zao
zitapatikana na kutumika. Vipaumbele vya kufanyika kwanza na kiasi cha kutumika
kwajili ya starehe na urembo kwa wanawake kwa mfano.
4. Masuala Ya Familia
Familia ya nani ianze kwanza na ipi ifuate ni tatizo kubwa
katika mahusiano. Upendeleo wa upande mmoja ambao kwa asili huwa unatokea tu ni
chanzo cha ugomvi ndani ya nyumba.
Mitazamo tofauti kati ya mmojawapo katika wapenzi na familia
ya mwenza wake husababisha kutoelewana kwa wapenzi hao ndani ya nyumba.
Mbaya sana inakuja pale wanandugu wanapoingilia mambo ya
ndani ya nyumba yenu. Wazazi wa kike na mawifi mfano, wamejulikana kusababisha
matatizo mengi kwenye familia za watoto na kaka zao.
Kuepukana na hili ni muhimu kwa wapenzi ndani ya nyumba
kuweka mipaka kwa ndugu ambayo haitaathiri uhusiano nao kama ndugu.
Pia ni muhimu kwa wenza hao kuweka mikakati ya pamoja juu ya
kuhusiana nakusaidia ndugu toka katika familia zao mbili.
5. Suala La Unyumba
Japo kuwa suala kufanya mapenzi si kila kitu kwa wapenzi
ndani ya nyumba lakini linachangia sana katika kuleta ugomvi aina yao. Kufanya
mapenzi kupita kiasi au mara chache kunaleta matatizo kwa wapenzi hasa ambao
wana uhitaji tofauti.
Wengine wanaona kama mpenzi ambaye hahitaji kufanya mapenzi
mara nyingi na mwenzake labda anauhusiano na mtu mwingine zaidi yake. Au hamvutii
tena kama zamani na huenda akaanza kuangalia nje.
Hii inajenga kutojiamini na kupoteza uaminifu,ambalo ni
tatizo jingine kubwa katika mahusiano kama tulivyoonesha mwanzoni.
6. Vipaumbele Katika Maisha
Wapenzi wawili wanapokuwa na mipango na malengo tofauti ni
tatizo kubwa. Watu wanapokuwa katika uhusiano ambao ni wa kuishi daima,malengo
na vipaumbele vyao ni lazima vioanishwe na juhudi za kila mmoja zilenge katika
kufanikisha mipango hiyo ya pamoja.
Kunapotokea kuwa kila mmoja ana malengo tofauti basi hata
vipaumbele vitakuwa tofauti na hapo ndipo shida zinapoanzia.
7. Uaminifu
Uaminifu katika mahusiaono ni jambo la muhimu sana. Bila
uaminifu ni ngumu sana kwa mahusiano yoyote kudumu.
Uaminifu ni kitu ambacho hujengwa kwa muda mrefu na
kikipotea ni ngumu sana kukirudisha. Japo inawezekana kujenga upya uaminifu
lakini huchukua muda mrefu sana.
8. Wapenzi, Marafiki Na Maisha Ya Zamani
Mojawapo ya vyanzo vya ugomvi kati ya wapenzi ni wapenzi wa
zamani. Mawasiliano ya aina yoyote na wapenzi wa zamani huleta wasiwasi mkubwa
kwa mpenzi wa sasa. Ni kitu ambacho wapenzi wawili wanahitaji kuongea na
kupanga jinsi ya kuepukana na matatizo ambayo yanaweza kusababishwa na historia
zao za maisha.
Kuepukana na hii ni vyema kuvunya uhusiano wa aina yoyote na
wapenzi wa zamani labda tu kama wapenzi hao ni wazazi wenza au mnafanya kazi
pamoja na ni ngumu kutokuonana au kuwasiliana.
Suala linalofanana na hili ni uhusiano na baadhi ya marafiki
wa jinsia moja ambao wanachukuliwa kuwa mfano mbaya na mpenzi wako. Kama haiwezekani
kutowasiliana na kuonana na wapenzi wa zamani au marafiki, basi ni vyema wakawa
marafiki wa familia nzima na mawasiliano yoyote kati yenu nao yawe wazi pasipo
kificho.
9. Watoto
Suala la uleaji na ukuzaji wa watoto linasababisha ugomvi
mara nyingi kati ya wazazi. Jinsi gani mtoto avae au shule ipi aende
linapelekea wazazi wengi kugombana.
Ni jambo la muhimu sana kukubaliana juu ya mambo ya msingi
juu ya malezi ya watoto. Tofauti za wazazi ziangaliwe kwanza vinginevyo
zitaingilia malezi ya watoto na kusababisha ugomvi juu yao.
10. Kazi Za Nyumbani
Imekuwa kama utamaduni kwa waafrika kuacha kazi nyingi kama
si zote za nyumbani kwa mke. Kwa Wanawake ambao wanafanya kazi pia inakuwa
ngumu sana. Hili linasababisha pia ugomvi kwa wapenzi nyumbani. Kama nguo
ambazo mume anazivaa na kuzichafua tu bila ya kujali kuwa mweza wake ataumia
wakati wa usafi na ikiwa yeye mwenyewe hajishughulishi na kufanya baadhi ya
kazi za nyumbani ni wazi itasababisha ugomvi.
Ni vyema wanaume kuchukua baadhi ya majukumu nyumbani hata
kama kutengeneza bustani au kulisha chakula mifugo.
No comments:
Post a Comment