
Wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi zilizopo katika kata
ya Mwangudo wilayani Meatu mkoani Simiyu wanasomea chini ya miti ikiwemo mibuyu
kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.
Shule hizo ikiwemo shule ya msingi Mbuyuni na Ng’ungulu
zenye idadi ya wanafunzi wanaokadiriwa kufikia zaidi ya 600 kila moja ina
vyumba viwili tu vya madarasa, matundu mawili ya vyoo na walimu wawili, mmoja
ni mwajiriwa wa serikali na mwingine ni mwalimu wa kujitolea ambapo mwalimu wa
zamu wa shule ya msingi Mbuyuni Emmanuel Robert ameiambia ITV kuwa uhaba wa
madarasa ni changamoto inayohitaji ufumbuzi wa haraka.
Akizungumzia kuhusu changamoto hizo, kaimu mkurugenzi wa
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Pamba Hezron
amewahimiza wananchi na viongozi wa vijiji kujenga vyumba vya madarasa na
nyumba za walimu huku akiahidi halmashauri kushughulikia tatizo la walimu na
vifaa vya kufundishia.
Nae meneja uhifadhi na maendeleo ya jamii wa makampuni ya
kitalii ya Mwiba holdings na TGTS Batro Ngilangwa amesema uhaba wa miundombinu
ya elimu katika shule zinazopakana na mapori ya akiba ya maswa na jumuiya ya
wanyamapori ya makao umezigusa taasisi hizo ambazo zimechangia ujenzi wa vyumba
vya madarasa na madawati.
No comments:
Post a Comment