Michezo miwili ya michuano ya kombe la klabu bingwa ulaya
katika hatua ya kumi na sita bora itachezwa leo nchini Ureno na Ufaransa.
Huko nchini Ureno Benfica watakua wenyeji wa Borussia
Dortmund kutoka nchini ujerumani mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Sport
Lisboa e Benfica, na mwamuzi wa mchezo huo ni Nicola Rizzoli raia wa Italia.
Mchezo wa pili utawakutanisha Paris Saint Germain ya
Ufaransa watakaokipiga na miamba wa Hispania Barcelona mchezo ukichezwa katika
dimba la Parc des Princes Jijini Paris.
Jumatano zitachezwa mechi nyingine mbili Bayern Munich
watachuana Arsenal na Real Madrid watatunishina misuli na Napoli ya Italia.
Mechi nyingine nne za michuano hii ya ulaya zitachezwa wiki
ijayo.
No comments:
Post a Comment