
Korea Kaskazini kwa mara nyingine tena imefyatua kombora na
kulielekeza upande wa Pwani ya Japan. Maofisa wa kijeshi kutoka Korea Kusini
wamekadiria kombora hilo limesafiri umbali wa takribani kilomita 500 huku
serikali ya Korea Kusini sasa imeitisha kikao cha kiusalama mjini Seoul .
Maafisa wa Pentagon nchini Marekani nao wamesema
wamelifuatilia tukio hilo na kuongeza kuwa wamebaini ni kombora la masafa ya
kadri.

Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini amesema vitendo kama
hivyo vya uchokozi unaoendelezwa na Korea Kazkazini vinaonyesha dhahiri jinsi
utawala jirani yao huyo usivyo na makini huku wakipania kuwa na zana za
Nuclear.
Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe ambaye angali ziarani
Marekani, ameshtumu ufyatuaji huo wa Kombora huku Rais Trump akimhakikishia Abe
kuwa anamuunga mkono asilimia 100.
Harakati hizo za ufyatuaji wa kombora zimekuja siku moja tu
baada ya mazungumzo kati ya rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa
Japan Shinzo Abe mjini Washington, ambako wamekubaliana kulipa kipa umbele
swala la jinsi ya kukabiliana na vitisho vya zana za kinuklia kutoka Korea
Kazkazini..
No comments:
Post a Comment