Msanii Rehema Chalamila a.k.a Ray C ambaye ametamba kwenye
anga la Bongo Fleva kwa siku nyingi, ameweka wazi kuwa kwa sasa hayuko kwenye
mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote.
Ray C ambaye amerejea kwenye game kwa kasi baada ya kutoka
kwenye dimbwi ya matumizi ya dawa la kulevya, amefunguka hilo alipokuwa kwenye
kipindi cha FNL cha EATV, na hakutaka kueleza sababu za kuamua kuishi bila
mpenzi.
Msanii huyo aliyewahi kutikisa na ngoma kadhaa za bongo
fleva zenye ujumbe wa mahaba kama vile Wanifuatia nini, Na wewe milele n.k
atatikisa jukwaa la Azura Jumanne katika usiku wa Valentine, ambapo amesema
amepania kutoa burudani kali kutokana na kukaa muda mrefu bila kufanya show,
Ameahidi kukata kiu ya wote waliokuwa wamem-miss huku
akiwataka kufika ukumbini hapo na wapenzi wao "Mimi ni mtu wa mapenzi,
nimetayarisha nyimbo nzuri, sijafanya show muda mrefu, nitaimba nyimbo zangu
kadhaa, na nawashauri kila mtu aje na mpenzi wake, ndiyo Valentine itanoga, pia
kutakuwa na kila aina ya burudani pamoja na dinner"
Kuhusu kurudi, amesema ana hamu ya kurudi kwenye game na
tayari amesharekodi nyimbo kadhaa, lakini alishauriwa aanze na Valentine kwanza
"Naendelea kurekodi, bosi wangu alinishauri nifanye
kwanza kwa ajili ya Valentine maana watu wanaulizia sana"

KUHUSU RECHO
Katika hatua nyingine, Ray C alitakiwa kutoa maoni yake
kuhusu Msanii Recho ambaye amekuwa akifuata nyayo zake kuhusu kutajwa kwake
kwenye orodha ya watu wanaohusika na dawa za kulevya, lakini alisema hawezi
kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hana uhakika juu ya suala hilo
"Mimi Recho namjua vizuri, lakini kutokana na matatizo
yangu sijaonana naye muda mrefu sana, sipo hapa kumzunguzia mtu, na siyo
vizuri, pia siyo vizuri kuzungumzia kitu ambacho sina uhakika nacho maana mimi
sijawahi kumuona akitumia hiyo kitu. Nachoweza kusema ni kuwa kama mimi
niliweza, kila mtu anaweza, naamini atakuwa poa maana najua ni mwanamke
imara" Amesema Ray C
No comments:
Post a Comment