Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameweka wazi sababu ya
kuteua mwanamke katika nafasi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kuwa ni
kutokana na kwamba wanawake wengi ni waaminifu katika suala la fedha.
Kamishna Jenerali Dkt. Anna Peter Makakala , Jenerali wa
Uhamiani Tanzania baada ya kiapo
Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 12 Februari,
2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kumuapisha Dkt. Anna Peter
Makakala kushika nafasi hiyo.
Mara baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amemtaka Kamishna
huyo kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Idara ya Uhamiaji nchini kutokana na
utendaji wake kutoridhisha.
Amiri Jeshi mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akimvisha cheo cha Jenerali Kamishna Dkt. Anna Peter
Makakala kabla ya kumuapisha kuwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania, Ikulu
Jijini Dar es salaam Februari 12,2016
“Nataka ukafanye mabadiliko makubwa (Total Reform), nataka Uhamiaji izalishe fedha kwa ajili ya nchi hii, nataka ukadhibiti utoaji hati za kusafiria (Passports) maana zimekuwa zikitolewa hovyohovyo..... Na kwenye suala la fedha simamia matumizi vizuri na kwa uaminifu, ndiyo maana katika nafasi hiyo nimekuteua wewe mwanamke maana najua wanawake ni waaminifu katika suala la fedha, ukishindwa unakuwa umewaangusha wanawake wote Tanzania ” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao pamoja na kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela, imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Kaimu Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Juma, Mawaziri, Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.
No comments:
Post a Comment