Rais wa Jamhuri ta Tanzinia Dkt John Magufuli, ameviagiza
vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya
dawa za kulevya kwa kuhakikisha vinasimamia sheria ipasavyo ili kukabiliana na
tatizo hilo nchini humo.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo hii leo katika Ikulu ya
mjini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuwaapisha Kamishna mkuu wa mamlaka ya
kupambana na kuzuia dawa za kulevya Bwana Rogers Siyanga, Kamishna Jenerali wa
uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji
Mheshimiwa Joseph Sokoine, Balozi wa Tanzania nchini Algeria Mheshimiwa Omar
Yusuf Mzee na Balozi wa Tanznia nchini Uganda Mheshimiwa Grace Aaron Mgovano.
#Dkt Magufuli amewataka viongozi wote wa serikali kuungana
na vyombo vya dola katika mapambano dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara
haramu ya dawa za kulevya, na ametaka mapambano hayo yasifanywe kwa mzaha wala
kwa kuangalia majina ya watu, vyeo vyao na taasisi wanazoongoza.
Mheshimiwa Magufuli amrwapongeza viongozi wote wa mikoa
walioanza kukamata watu wanaojihusisha na biashara za dawa za kulevya, na
amewaomba Watanzania wote waunge mkono juhudu za kukabiliana na wanaofanya
biashara na kutumia dawa za kulevya, ambazo zinazidi kuangamiza nguvu kazi ya
taifa.
No comments:
Post a Comment