Msanii wa muziki Q Chief amedai kuwa jina lake halikutajwa
katika list ya RC Makonda kwa kuwa yeye tayari alishaachana na matumizi ya
Madawa ya kulevya.
Muimbaji huyo amedai kutembea au kukaa na watu ambao
wanatumia Madawa ya kulevya haimaanishi kwamba na yeye bado anaendelea kutumia.
“Mimi siko kwenye hiyo list na nilishaacha hizo mambo,” Q
Chief alikiambia kipindi NLF cha EATV. “Ningekuwa natumia ungekuta jina langu
kwenye list ya Makonda lakini mimi siko,”
Aliongeza, “Mimi ni mtoto wa uswahilini, nimekuwa huko kwa
hiyo kutembea au kuonekana maeneo ambayo wanakaa wahumi ni maeneo yangu kwa
sababu ndiko waliko washkaji zangu,”
Q Chief alidai yeye aliweza kuacha mwenyewe matumizi ya
Madawa ya kulevya baaada ya kuona yanampotezea mwelekeo katika maisha yake.
No comments:
Post a Comment