Mwanamke mmoja alikatiza mkutano wa umma uliokuwa
umehudhuriwa na Rais wa Tanzania John Magufuli kwenye mji mkuu wa Dar es
Salaam, kumuomba achukue hatua dhidi ya watu ambao amewalaumu kwa kupanga njama
ya kumnyanganya mali yake.
Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina Shosi, alizua kizaa zaa
wakati wa siku ya sheria ambayo ni warsha ya kila mwaka, inayoandaliwa na
mahakama kutoa mafunzo ya kisheria na misaada ya sheria.
Kwenye video iliyosambazwa katika mitandao, mama huyo
alibeba bango lenye maandishi lililosababisha Rais Magufuli kuwaamrisha polisi
kumruhusu aende karibu na eneo alikuwa ameketi.
Bi Shosi kisha akaanza kuelezea jinsi mifumo ya mahakama
imehujumu kesi yake kwa kutoa amri zinazokinzana na kuwa amapokea vitisho kwa
maisha yake.
Gazeti la serikali la Daily News, linaripoti kuwa Bi Shosi
ni mjane raia wa Kenya ambaye alikuwa ameolewa na raia wa Tanzania na aliishi
mkoa wa Tanga.
Bwana Magufuli aliwaamrisha majaji kwa haraka kusikiliza
kesi yake. Pia alimuamrisha jaji mkuu ambaye alikuwa kwenye mkutano huo kumpa
mama huyo namba yake ya simu ili waweze kufuatilia naye kesi hiyo.
Pia magufuli alimuarisha mkuu wa polisi kuhakikisha kuwa Bi
Shosi amepewa ulinzi wa kutosha.
No comments:
Post a Comment