Watuhumiwa wa biashara na matumizi ya dawa za kulevya
waliotajwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaamm, Paul Makonda,
Jumanne hii, February 7, 2017 wamefikishwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar
es Salaam kujibu tuhuma zinazowakabili.
Mastaa hao wakiwemo TID, Nyandu Tozi, Babu wa Kitaa, Romy
Jones, Tunda, na wengine, wameachiwa kwa sharti la dhamana ya shilingi milioni
10 kila mmoja na watakuwa wakiripoti kwa mwezi mara mbili huku wakiwa katika
uangalizi wa jeshi la polisi kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Hata hivyo watuhumiwa wengine wakiwemo Petit Man, Said
Alteza, Lulu Diva na wengine wametakiwa kuweka dhamana ya shilingi milioni 20
na watakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka mitatu. Iwapo watuhumiwa
hao watashindwa kufuata masharti hayo watarudishwa tena mahakamani.
Hali imekuwa tofauti kwa Wema Sepetu ambaye ameendelea kukaa
rumande baada ya msako kubaini msokoto wa bangi nyumbani kwake na hivyo
kuongezwa kosa jingine zaidi ya lile la awali, ambapo sasa inasubiriwa
uchunguzi kukamilika.
No comments:
Post a Comment