Misri imeweka rekodi kwa kufanikiwa kufuzu kwa mara ya tisa
katika fainali za kombe la Afrika baada ya kuishinda Burkina Faso 4-3 katika
mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1.
Mlinda lango wa miaka mingi Essam El Hadary alithibitisha
ushujaa wake kwa kuokoa penalti iliopigwa na Betrand Traore ili kupata ushindi
huo.
Wakati wa muda wa kawaida Mohamed Salah aliiweka kifua mbele
Misri baada ya kufunga bao zuri.
Hatahivyo Burkina Faso walisawazisha wakati Aristide Bance
alipofunga krosi iliopigwa na Charles Kabore.
Kupitia bao hilo Burkina Fasso imekuwa timu ya kwanza
kuifunga Misri katika mchuano huo.
Wachezaji wa Burkinabe ambao ndio walioonyesha mchezo mzuri
wakati wa muda wa kawaida walianza penalti hizo kwa kufunga, lakini Misri
ikaibuka mshindi baada ya Traore kushindwa kucheka na wavu.
No comments:
Post a Comment