Chelsea ililazimika kutoka sare dhidi ya timu ya Liverpool
ilioimarika katika uwanja wa Anfield baada ya penalti ya Diego Costa
kupanguliwa na kipa Simon Mignolet lakini bado wakaongeza uongozi wao katika
kilele cha ligi ya Uingereza na pointi tisa.
Kipa wa Liverpool Mignolet alirekebisha makosa yake baada ya
kupatikana amezubaa na mkwaju wa adhabu wa David Luiz.
Kichwa cha karibu cha Georginio Wijnaldum kunako dakika ya
11 baada ya muda wa mapumziko kiliipatia Liverpool sare waliohitaji, na
hivyobasi kusitisha msururu wa matokeo mabaya ambao ulikuwa umekumba timu hiyo.
Matokeo hayo yalisababisha kubanduliwa kwa timu hiyo katika
kombe la EFL pamoja na lile la FA.
Hatahivyo ingekuwa bora zaidi kwa Chelsea na vibaya zaidi
kwa Liverpool baada ya Costa kuangushwa na Joel Matip dakika 14 kabla ya
kukamilika kwa mtanange huo.
Refa Mark Clattenburg alitoa penalti kwa upande wa Chelsea
lakini kipa Mignolet akaokoa penalti hiyo.
No comments:
Post a Comment