
Watu saba wanahofiwa kufa maji katika Ziwa Tanganyika baada
ya boti ya MV Ngendo Buchuma waliyokuwa
wakisafiria ikiwa na tani 20 za mzigo
kutoka mjini Kigoma kwenda mji wa Kalemie Jamhuri ya Kidemokrasi ya watu
wa Kongo kutoonekana kwa zaidi ya wiki moja sasa.
Mwenyekiti wa umoja wa wasafirishaji maboti Kigoma Uwamaki
Edmud Kisinja amesema boti hiyo ikiwa na wafanyakazi wanne na wamiliki watatu
wa mzigo wa vitunguu gunia 110,soda
kreti 70,mafuta pipa 20 na ngano mifuko 180, waliondoka tarehe 23 mwezi wa
kwanza lakini mpaka sasa hawajulikani walipo huku jitihada zikiwa zimefanywa
kuwatafuta Mashariki ya DRC pamoja na upande wa Tanzania bila mafanikio hali
inayoashiria huenda boti hiyo ambayo ilipaswa kutumia kati ya masaa 12 hadi 24
kufika DRC,imezama ziwani.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma kamishna
Msaidizi Mwandamizi Ferdinand Mtui amesema mpaka sasa hawajapata taarifa zozote
kuhusiana na boti hiyo wala kuona mabaki ya mzigo wala miili ya watu na
jitihada zinaendelea.
No comments:
Post a Comment