Klabu ya Barcelona kwa sasa ina matumaini tele kufuatia beki
wake mahiri Gerard Pique kuanza mazoezi wakati wakielekea katika mchezo wao wa
kesho wa nusu fainali ya mkondo wa pili ya Kombe la Mfalme dhidi ya Athletico
Madrid.
Beki huyo alilazimika kutolewa wakati wa mapumziko katika
ushindi wa mabao 3-0 waliopata Barcelona dhidi ya Athletic Bilbao Jumamosi
iliyopita baada ya kupata majeruhi ya msuli.
Meneja wa klabu hiyo Luis Enrique amesema majeruhi hayo ya
Pique yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na ratiba ngumu waliyonayo.
Hata hivyo, nyota huyo wa kimataifa wa Hispania alifanya
mazoezi na wenzake mapema leo na kuna kila dalili atakuwepo katika mchezo huo
wa kesho ambao Barcelona wanaongoza kwa mabao 2-1 waliopata katika mchezo wa
mkondo wa kwanza.
No comments:
Post a Comment