Rais John Pombe Magufuli amemteua Luteni Jenerali Venance
Mabeyo kuwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania akichukua mahala pake
jenerali Davis Mwamunyange aliyestaafu.
Taarifa kutoka ikulu iliotumwa katika vyombo vya habari
inasema kuwa Luteni huyo sasa amepandishwa cheo na kuwa jenerali kamili.
Wakati huohuo rais amemteua meja jenerali James Mwakibolwa
kuwa mnadhimu mkuu wa majeshi ya ulinzi akichukua mahala pake Jenerali
Mabeyo.Pia yeye alipandishwa cheo cha luteni jenerali.
Rais amesema kuwa uteuzi huo unaanza kutekelezwa mara moja.
Tarehe ya kuapishwa kwa wawili hao itatangazwa baadaye.
No comments:
Post a Comment