Barcelona wameifunga Atletico Madrid katika mzunguko wa
kwanza wa nusu fainali ya kombe la Copa del Rey katika dimba la Vicente
Calderon.
Katika mchezo huo ulioisha kwa Atletico Madrid kuchapwa 2-1
huku magoli ya Barcelona yakifungwa na Messi pamoja na Suarez na lile la
Atletico likipachikwa na Griezman, ilishuhudiwa Messi akifikisha magoli 200
katika michezo 274 ya ugenini.
Mchezo wa marudiano utakuwa Februari 7 ambapo Barcelona
itakuwa katika dimba lake la nyumbani Camp Nou.
Alaves na Celta Vigo ni timu nyingine ambazo zitachezaa nusu
fainali Februari 8.
No comments:
Post a Comment