Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye
aliwaongoza mashabiki lukuki wa Singida kuishangilia timu yao ya Singida United
ambapo imefanikiwa kupanda ligi kuu msimu ujao baada ya kuifunga Alliance 2-0
amesema, Singida United itakuwa kama Leicester City ya England ambayo ilipanda
ligi kuu na kutwaa taji la ligi kwa kuvibwaga vigogo.
“Ninafuraha sana kama ambavyo unawaona wanasingida, hili ni
jambo ambalo limesubiriwa kwa miaka mingi sana na sisi kama wadu wa mkoa wa
Singida tutaendelea kuunga mkono timu yetu ya mkono timu yetu ya mkoa ili iweze
kufanya vizuri zaidi,” – Mwigulu Nchemba.
“Nawatakiwa kila la heri wana Singida, tuendelee kuiunga
mkono timu yetu ya Singida United. Msimu ujao Singida United itakuwa kama
Leicester City, inaenda kuchukua ubingwa.”
Nchemba ni mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi na mdau
mkubwa wa soka nchini akiziunga mkono Singida United ya mkoani Singida pamoja
na Yanga SC.
No comments:
Post a Comment