Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kwa
kosa la kupatikana na dawa za kulevya yanayodhaniwa kuwa heroine kiasi cha
pinchi 240 na ndonga mbili.
Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa leo, imedai kuwa mtu huyo
aliyejulikana kwa jina la Kassim Hemed Kesi mwenye umri wa miaka 43, amekamatwa
majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Kanyerere kata ya Butimba
wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza.
Taarifa hiyo imedai kuwa mtu huyo ni mfanyabiashara wa spear
za magari katika mtaa huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema
kuwa awali polisi walipata taarifa za mtuhumiwa huyo kuwa anajihusisha na
biashara ya madawa ya kulevya, hivyo askari walikuwa wakiendelea na upelelezi
pamoja na uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo.
Aidha wakati askari wakiendelea na upelelezi dhidi ya tuhuma
za mfanyabiashara huyo, jana tarehe 09.02.2017, polisi walipokea taarifa kutoka
kwa raia wema kwamba mtuhumiwa huyo ameingiza mzigo mkubwa wa madawa ya kulevya
kutoka Dar es Salaam na ameanza kuusambaza mtaani.
Tukio lilivyokuwa
Askari walianza kufanya ufuatiliaji wa haraka kuhusiana na
taarifa hizo, ndipo ilipofika majira ya saa sita usiku askari walifika hadi
nyumbani anapoishi mtuhumiwa na kuizingira nyumba yake yote na kumuona kupitia
dirisha akiendelea kufunga madawa hayo kwenye vikete vidogovidogo maarufu kama
pichi.
Wakati askari wanataka kuingia ndani ya nyumba mtuhumiwa
alishtuka na kukimbiza mzigo huo wa madawa ya kulevya chooni ili kupoteza
ushahidi.
Aidha askari waliona kitendo kile kupitia dirishani na
baadhi YA askari waliingia ndani na kufanikiwa kukuta pinchi 240 zikiwa chooni
lakini bado hazikuwa zimetumbukia shimoni na kufanikiwa kuzitoa kwenye tundu la
choo.
Msangi amesema wakati huohuo askari wengine waliokuwa nje
walikwenda kuvunja bomba linalopitisha uchafu/choo linalokwenda kwenye shimo na
kuweka kizuizi hapo na kufanikiwa kupata ndonga 2 za dawa za kulevya huku
nyingine zikibebwa na maji .
Polisi wanaendelea na mahojiano na mtuhumiwa ili kuweza
kubaini mtandao wa watu aliokuwa akijihusisha nao katika biashara hiyo ya
madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment