
Mtangazaji wa kipindi cha Ala za
Roho cha Clouds FM, Diva The Bosslady amefunguka kwa kudai kuwa katika mastaa
wa muziki Alikiba ndiye msanii ambaye anatamani kudate naye.
Diva ambaye kwa sasa anatoka
kimapenzi na muimbaji Heri Muziki, alikuwa host wa show ya Valentine’s Day
iliyofanyika Jumatano hii katika ukumbi wa Next Door na kuhudhuriwa na mastaa
mbalimbali.
Akiongea na waandishi kabla ya
kwenda kusherehesha show hiyo iliyoandaliwa na Irene Uwoya, Diva alidai Alikiba
ndiye msanii ambaye anatamani kudate naye

“Alikiba ndiyo msanii au staa
ambaye natakamani kudate naye,” Diva alisema baada ya kuulizwa ni staa gani
ambaye anatamani kudate naye. “Sijawahi kutoka naye kimapenzi, pia sasa hivi
mimi nipo kwenye mahusiano na mtu mwingine,”
Mtangazaji huyo alidai yeye
wanaume wake wengi anawapata kupitia kipindi chake la Ala za Roho ambacho
huchambua mambo mbalimbali kuhusu mahusiano.
No comments:
Post a Comment