
Msanii wa bongo movie Wastara
amemchana mpenzi wake wa sasa Bond kwamba asipojirekebisha baadhi ya tabia zake
atamuacha na akimwacha hatarudi tena kwake.
Hata hivyo Wastara amesema
anaweza kuvumilia shida anazopata kwa Bond lakini anaweza kumuacha muda wowote
kwani hahitaji 'stress' za kimapenzi huku akiweka wazi kuwa amejitahidi na
amefanikiwa kumrekebisha kwa 80 % na endapo ataendelea na mambo yake ya zamani
zamani ataachana naye.
Akiongea kupitia eNewz ya EATV,
Wastara amesema "Niseme tu ukweli kwamba kwa Sajuki hakuna mtu anayeweza
kufikia upendo wetu kwa kuwa Sajuki alikuwa anajali kila kitu ambacho nilikuwa
nakipenda, kitu ambacho mpaka sasa sijapata ni mtu ambaye amefikia hatua za
Sajuki ". Alisema Wastara.
No comments:
Post a Comment