Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye wametangaza
kuufungua tena uwanja wa taifa baada ya kuufunga mwezi Oktoba mwaka jana kwa
shughuli zozote.
Uwanja huo ulifungwa kutokana na uharibifu uliotokea wakati
wa vurugu zilizotokea uwanja huo wakati wa mechi ya watani wa jadi Simba na
Yanga iliyochezwa Oktoba 1 mwaka jana. Uwanja huo utaanza kutumika katika mechi
ya Simba na Azam itakayochezwa Jumamosi hii.
Soma taarifa hiyo zaidi hapa chini.
No comments:
Post a Comment