Baadhi ya watu wanadai kwenye ngoma hiyo wanamsikia Zilla
ambaye hawajamzoea. Lakini kwa rapper huyo wa Salasala, mapokeo ya aina hiyo ni
kitu anachokitarajia sababu anafahamu kuwa anahudumia kundi kubwa lenye
interest zinazopishana.
“Unajua biashara yetu tunadeal na watu wengi so kila mtu na
views zake. Unajua kila mtu akikuona wewe, kuna kitu anatarajia kutoka kwako,”
“Unajua ‘too much is given, much is tested’ aliyebarikiwa
haachi kujaribiwa, unajua mtu unaimba nyimbo kama ‘waiter leta mitungi’ kuna
mlevi alishazoea party anataka upige kama ile. Halafu unapiga labda ‘Mungu ni
mwema’ kuna mtu wa gospel kesho anataka utoe kama hii. Kwahiyo unatoa huduma
kwa watu wengi ambao kila mtu anataka kukusikia kwa angle yake aliyowahi
kukusikia, it’s impossible,” amesisitiza.
No comments:
Post a Comment