Msanii wa muziki Ommy Dimpoz amedai licha ya yote
yaliyotokea kati yake na Diamond Platnumz, lakini anaweza kuingia studio na
kufanya kolabo na msanii yeyote wa WCB kama ikitokea kazi ambayo itamwitaji
kufanya hivyo.
Wawili hao ambao walikuwa marafiki wa muda mrefu,
waligombana na kufikia hatua ya kutupiana maneno ya kashfa kupitia mitandao ya
kijamii.
Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Ijumaa
hii, Ommy amedai kama ikitokea kazi ambayo ataona anatakiwa kufanya na msanii
wa WCB basi atamtafuta kwa kuwa muziki ni biashara.
“Sio Nedy hata mimi naweza kufanya kolabo na wasanii wa WCB
kwa sababu mwisho wa siku hii ni biashara, unapoona hapa anatakiwa kukaa
masanii fulani unamtafuta ili kupata kitu kizuri zaidi,” alisema Ommy Dimpoz.
Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Kajiandae’
akiwa ameshirikiana na Alikiba.
No comments:
Post a Comment