Geita. Wachimbaji 15 waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya
Mkoa wa Geita kwa ajili ya matibabu baada ya kuokolewa katika mgodi wa RZ
walikokuwa wamefunikwa na kifusi cha udongo kwa siku tano wameruhusiwa kutoka
hospitali baada ya afya zao kuwa nzuri.
Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Brian Mawala amesema afya za
wachimbaji hao zimeimarika na wana uwezo wa kuendelea na kazi.
Baada ya kuruhusiwa leo asubuhi wamekutana na Mkuu wa Mkoa
wa Geita, Ezekiel Kyunga.
No comments:
Post a Comment