Kiungo wa kati wa timu ya Arsenal Mohamed Elneny anakabiliwa
na jukumu la kuhakikisha ana kuwa sawa kiafya ili kushiriki katika fainali za
michuano ya kombe la mataifa ya Afrika maarufu AFCON, endapo nchi ya Misri
itafanikiwa kufika hatua hiyo.
Elneny ni miongoni mwa wachezaji wakali wa Misri na tayari
amekumbwa na tatizo la kifua wakati wa mchezo wa nusu fainali wakati timu yake
ilipomenyana na Morocco.
Meneja wa timu timu ya Misri Ihab Lehata amethibitisha kuwa
Elneny huenda asiingie uwanjani tena katika michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment