Bingwa wa mbio za mita 100 upande wa wanaume Usain Bolt
atalazimika kurudisha dhahabu moja miongoni mwa dhahabu tisa alizoshinda baada
ya mwanariadha mwenza Nesta Carter kupatikana alitumia dawa za kusisimua
misuli.
Carter alikuwa miongoni mwa wanariadha wanne wa Jamaica
walioshinda mbio za mita 100 kupokezana vijiti katika michezo ya beijing 2008.
Ni miongoni mwa wanariadha 454 waliochukuliwa violezo vyao
na kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC mwaka uliopita na amepatikana alitumia
dawa ya aina ya methylhexaneamine.
Bolt mwenye umri wa miaka 30 alishinda dhahabu tatu katika
michezo ya Olimpiki ya Rio msimu uliopita.
Alishinda dhahabu katika mbio za mita 100, 200 na 400
kupokezana vijiti na kuongeza mafanikio yake katika mbio hizo mwaka 2008 na
2012.
Carter mwenye umri wa miaka 31 alikuwa miongoni mwa
wanariadha walioshinda dhahabu katika mbio hizo mjini London miaka mitano
iliopita na kuisadidia Jamaica katika mbio za dunia miaka ya 2011, 2013 na
2015.
Alikuwa wa kwanza kukimbia katika mbio za rilei za 4 mara
100 mjini Beijing ambazo zilimuhusisha mwanariadha Michael Frater, Asafa Powell
na Bolt.
Jamaica ilishinda kwa kuvunja rekodi ya dunia baada ya
kumaliza kwa sekunde 37.10 mbele ya Trinidadad and Tobago na Japan ,ambao sasa
medali zao zitaongezwa.
Brazil itajipatia medali ya shaba.
No comments:
Post a Comment