Jengo la ghorofa tatu lilokuwa katika ukarabati katika
Mjimkongwe wa Zanzibar limeporomoka na
kuua mtu moja na mwengine kujeruhiwa
vibaya.
Jengo hilo la ghorofa tatu ambalo liko katika mtaa wa
Mjimkongwe lilianguka wakati mafundi
wawili wakiwa wako kazini na ghafla ukuta wa mbele ukaporomoka na kuwatupa
barabarani ambapo moja ya fundi huyo,
aliokolowa na wananchi na kumpeleka hospitali kuu ya Mnazimoja huku hali yake ikiendelea kuwa nzuri ,lakni
pamoja na jitihada za kikosi cha ziamamto na wananchi kujaribu kumuokoa fundi
mwingine hazikufanikiwa na fundi huyo
alifariki baada ya kufukuliwa na kikosi hicho na maiti yake kupelekwa hospitali kuu ya
Mnazimoja kwa uchunguzi kabla ya familia
kukabidhiwa kwaajili ya maziko ambapo kamanda wa polisi Mjinimagharibi Kamishna
Msaidizi mwanadamizi wa polisi Hassan Nasser alithibitisha kutokea kwa ajali
hiyo.
Wakizumgumza
mashuhuda walioshudia jengo hilo likiporomoka ambalo ni mali yawakfu na mali amana wamesema
ilikuwa ni mshutko mkubwa ambao
uliwashtua wananchi wa hapo lakini bahati nzuri hapakuwepo na wapita njia
wakati udongo na mawe yakiporomoka ingawa ni pikipiki moja iliyokuwa
imeegemezwa ilifunikwa huku injinia wa
mamlaka ya Mjimkongwe Mussa Awesu Bakari
amesema ujenzi wa jengo hilo ulikuwa unafanyika kwa mujibu wa sheria na
taratibu zote za mamlaka ya Mjimkongwe.
No comments:
Post a Comment