
Kwa mujibu wa The
Independent na ParsToday wanasema kuwa Rais Donald Trump wa Marekani amewafuta
kazi mabalozi wote wa nchi hiyo kote duniani na wanaohudumu katika mashirika ya
kimataifa ambapo uamuzi huo umefanyika katika siku yake ya kwanza kazini.
Trump ambaye aliapishwa Ijumaa January 20, 2017 kuwa Rais wa
45 wa Marekani, amewataka mabalozi wote walioteuliwa na mtangulizi wake, Barack
Obama kuondoka kazini mara moja bila hata kuwapa muda wa kujitayarisha kuondoka
kama ilivyo kawaida.
Inaelezwa kuwa zaidi ya mabalozi 80 wa Marekani katika nchi
mbalimbali duniani walifutwa kazi Ijumaa tarehe 20 Disemba saa sita mchana
ikiwa ni mara baada ya Trump kuapishwa.
Hatua hiyo ya Trump inatazamiwa kuvuruga uhusiano na
washirika muhimu kama vile Ujerumani, Uingereza na Canada ambapo ripoti zinasema
nchi hizo zinaweza kukaa bila mabalozi kwa miezi kadhaa kwani baada ya Trump
kuteua mabalozi wapya watalazimika kuidhinishwa na Bunge la Congress kabla ya
kuanza kazi zao.
Donald Trump anakosolewa kwa kuacha nafasi nyingi wazi na
hivyo kuvuruga shughuli za kawaida za serikali ya Marekani na hii haya yanajiri
huku maandamano yakiripotiwa kuendelea sehemu mbalimbali kupinga utawala wa
kiongozi huyo.
Nchini Marekani katika siku ya pili ya utawala wa Trump
kumeripotiwa maandamano ya watu milioni tatu na imeripotiwa kumefanyika
maandamano 637 katika maeneo mbalimbali ya Ulaya, Asia na Afrika kumpinga rais
mpya wa Marekani.
No comments:
Post a Comment