MSHAMBULIAJI wa Tanzania
Thomas Ulimwengu amesajiliwa
na timu ya Ligi Daraja la Kwanza Nchini
Sweden inaitwa Athletic Football Club Eskilstuna kwa mkataba miaka miwili
Baada ya mkataba wake ulimalizika, Ulimwengu hakutaka kuongeza mkataba mwingine na kusema
malego yake ni kutaka kucheza Ulaya.
Ulimwengu alisema: “Kweli nimesajiliwa kwa mkataba wa miaka
miwili kuitumikia timu hiyo ambayo nitajiunga nayo hivi karibuni”
“Kwa sasa nashughulikia mambo ya visa kuanzia wiki
ijayo nitaenda nimeshajiunga na timu ya
Athletic Football Club Eskilstuna ya
Sweden.”
Ligi hiyo ya daraja la Kwanza inashirikisha timu kumi na nne
na inatarajia kutimua vumbi April kumi na nne mwaka huu.
No comments:
Post a Comment