
Staa wa soka wa kimataifa wa Argentina aliyewahi kuchezea
timu za West Ham United, Man United na Juventus Carlos Tevez amewasili China
baada ya siku kadhaa nyuma kusaini mkataba wa kujiunga na timu ya Shanghai.

Tevez anawasili kujiunga na timu
hiyo akiwa kavunja rekodi ya kulipwa mshahara ya Lionel Messi wa FC Barcelona
na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambao ndio walikuwa wachezaji wanaoongoza
kulipwa mshahara mkubwa zaidi duniani kabla ya Oscar na Tevez kujiunga na
Shaghai.a

Hivyo kwa sasa Tevez ndio atakuwa
mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani akifuatiwa na Oscar
aliyejiunga na Shaghai pia akitokea Chelsea, kwa wiki Tevez atakuwa akilipwa
mshahara wa pound 615000 ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 1.6 za kitanzania.






List ya wachezaji wanaolipwa
mishahara mikubwa zaidi duniani Tevez na Oscar ndio wanaoongoza.
No comments:
Post a Comment