SERIKALI imesema hakuna binadamu yeyote aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa wa mafua ya ndege nchini.
Akizungumza katika
mahojiano maalumu jana, Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema hakuna
mgonjwa yeyote aliyepatikana na ugonjwa huo nchini hadi sasa.
Ummy alisema hayo akitoa ufafanuzi baada ya kuenea uvumi
kwamba kisiwani Zanzibar, amepatikana mgonjwa mwenye mafua ya ndege.
Alisema kutokana na kuibuka kwa ugonjwa huo nchi jirani
serikali imetuma watalaamu mpakani mwa Tanzania na Uganda kutoa elimu kwa
wananchi namna ya kujihadhari na ugonjwa huo.
Aliwataka madaktari wote nchini wakimwona mgonjwa mwenye
dalili au mafua yasiyo ya kawaida, kumpima na kumpa tiba haraka kabla hajaugua
au hajaambukiza.

No comments:
Post a Comment