
Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe ametembelea shamba lake la
kilimo cha kisasa cha mboga mboga (Green House) yaliyopo Hain na kuwajulia hali
wafanyakazi pamoja na wataalam wake leo Ijumaa.
Pia, Mbowe amepata wasaa ya kuzungumza na baadhi ya
wafanyakazi ambao walimweleza hofu kubwa waliyoingiwa nayo ya kupoteza ajira zao wanazozitegemea
katika kuendesha maisha yao ya kila siku.
Hali hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasiu
Byakanwa kupiga marufuku shughuli za kilimo zinazoendeshwa na shamba la Kilimanjaro
Veggies linalomilikiwa na Mbowe.
Byakanwa alitoa amri hiyo baada ya kutembea shamba hilo
lenye ukubwa wa hekari mbili akisema kilimo hicho ni kinyume cha sheria kwani
shamba hilo lipo ndani ya mita 60 kutoka mto Weruweru.
No comments:
Post a Comment