Wiki iliyopita mcee mkongwe nchini, Fid Q alizua maswali
mengi baada ya kuonesha kuupa heko wimbo mpya wa Joh Makini,Waya, mkali ambaye
tulikuwa tukiamini kuwa wana tofauti.
Sasa mbali na ngoma hiyo ya Joh Makini,Fid Q ameitaja ngoma
ya Sinaga Swagga ya Young Killer kuwa ni ngoma ambayo ameisikiliza sana pia.
“Nimeiskia Sina Swagga ya Young Killer,nimeipenda, nimependa
jinsi ambavyo amejaribu kuwa yeye,” Fid kwenye mahojiano nami kupiti Kings FM.
Kwa muda mfupi wimbo huo wa Young Killer ulisababisha
headlines kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuwachana rappers
wenzake wakiwemo Joh Makini, Young Dee na Dogo Janja.
By Prince Ramalove
Kings Fm
No comments:
Post a Comment