Wachezaji wa klabu ya West Ham walitaka Dimitri Payet
kuondoka katika klabu hiyo kabla ya kuelekea Mersaille ,kulingana na mwenyekiti
mwenza wa klabu hiyo David Sullivan.
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29
alijiunga tena na klabu yake ya zamani kwa kitita cha pauni milioni 25 baada ya
kudaiwa kukataa kuichezea West Ham kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
''Kwa kweli hatukutaka aondoke lakini huwezi kwenda kinyume
na umoja wa timu'' ,sullivan
Sullivan alisema kuwa Payet aliamua kutochukua mshahara wake
wa Januari.
''Payet hakuzungumza na mtu kwa wiki sita.Amekataa
kuzungumza na mtu yeyote katika timu'',alisema Sullivan.
Payet alijiunga na West Ham mwezi Juni 2015.
No comments:
Post a Comment