Bocco ndiye mshambuliaji pekee nchini mpaka sasa aliyeweza
kuzitesa timu za Simba na Yanga kwa kufunga mabao, kila anapokutana nazo katika
mechi mbalimbali.
Ukiondoa rekodi ya kuifunga Yanga jumla ya mabao 12, Bocco
mpaka sasa amefanikiwa kutikisa nyavu za Simba mara 18 katika mechi za
mashindano mbalimbali ambapo John Bocco kutoka Azam FC leo ameisaidia timu yake
ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba Sport Club katika uwanja wa
Taifa Jijini Dar es Salaam. Na kumfanya awe ametikisa nyavu za Simba mara 19.
Bocco aliingia kwenye mchezo huo dhidi ya Simba akiwa na morali kubwa ya kuendeleza rekodi
yake ya kufunga kwani katika mechi ya mzunguko wa kwanza msimu uliopita
alitupia mawili kwenye sare ya 2-2, huku ya wekundu hao yakifungwa na Ibrahim
Ajib.
No comments:
Post a Comment