
Prisons imeendeleza ubabe wake kwa Mbeya City baada ya
kuitwanga kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine
mjini Mbeya, leo.
Prisons ilionyesha soka safi tokea mwanzo, lakini Mbeya City
wakafanya mashambulizi mengi ingawa kipa wa Prisons akawa kipingamizi kikubwa
kwao kupata bao.
Wakati Prisons wakiitwanga Mbeya City, upande mwingine mechi
iliyokuwa ipigwe Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kati ya wenyeji Ndanda FC na
Majimaji
Majimaji ambao ni majirani wa Ndanda, walichelewa kufika
mjini Mtwara na sasa mechi hiyo itapigwa kesho.
No comments:
Post a Comment