Mbunge mmoja nchini Kenya amewasilisha mswada bungeni
kuzishinikiza kampuni zinazouza pombe kutoa asilimia ndogo ya faida yao
kuwadhamini wanywaji ambao wataathirika na pombe hiyo.
Mbunge Gideon Mwiti anataka watengenezaji wa pombe kutoa
kati ya asilimia 5 na 10 ya mapato wanayopata kwa kampuni za bima ili kuwafidia
watu ambao wataathirika na pombe ama hata kupata ajali kwa kuwa walevi
kulingana na gazeti la Daily Nation nchini humo.
Mswada huo pia unapendekeza kwamba iwapo mtu atafariki
kutokana na athari za kunywa pombe ,kampuni hizo za pombe zilazimike kufidia
familia yake.
Bw Mwiti pia amezishutumu kampuni za pombe kwa kushindwa
kukuza pombe zisizo na madhara kwa afya, kwa mujibu wa ripoti hiyo.
No comments:
Post a Comment