Klabu ya ligi ya La Liga Celta Vigo imewalaza viongozi wa
ligi hiyo Real Madrid na kufika katika nusu fainali ya kombe la Copa del Rey
baada ya kutoka sare ya 2-2 na hivyobasi kufuzu kwa jumla ya mabao 4-3.
Wenyeji Celta Vigo ndio waliokuwa wa kwanza kucheka na wavu
baada ya muda wa kupumzika kupitia beki Danilo aliyejifunga.
Christiano Ronaldo hatahivyo aliwasawazishia wageni baada ya
kupiga mkwaju wa adhabu kabla ya Daniel Wass kuiweka kifua mbele Celta Vigo.
Lucas Vazquez alifunga bao la pili kwa kichwa lakini
halikuisaidia Real Madrid.
Msururu wa matokeo mazuri ya kutofungwa kwa upande wa klabu
ya Real Madrid ulisitishwa na Sevilla mapema mwezi Januari.
Wameshinda mara moja katika mechi zao tano katika mashindano
yote.
No comments:
Post a Comment