Msanii wa muziki kutoka WCB, Queen Darleen amekanusha uvumi
ambao waliwahi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa alikuwa anatoka
kimapenzi na msanii Alikiba.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Kijuso,
amesema mara nyingi watu wakiona anakuwa karibu na mtu fulani huwa wanahisi
kuwa ni mtu wake.
“Alikiba siyo bwana wangu na wala hajawahi kuwa bwana wangu,
ila Alikiba alikuwa mshikaji wangu na zaidi ya mshikaji wangu, yaani ni ndugu
kabisaa, hivyo watu waliweza kuona natoka naye kwa kuwa nilikuwa karibu naye,
nazunguka naye mara kwa mara karibu sehemu zote, hivyo watu wakawa wanajua
hivyo na hiyo ni kutokana na ukweli kwamba watu walikuwa hawamjui bwana wangu.”
Queen Darleen alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Muimbaji huyo alizidi kufafanua na kusema kama kweli
angekuwa anatoka kimapenzi na Alikiba kipindi hicho basi hata mtoto wake
angekuwa ni mtoto wa Alikiba.
“Kipindi kile nazurula sana na Alikiba mimi nilikuwa tayari
mjamzito, na nisha jifungua na mtoto kwa mantiki hiyo kama Alikiba angekuwa
bwana wangu basi yule mtoto angekuwa wa Alikiba, lakini mimi nilikuwa na
mwanaume wangu kipindi hicho ambaye ni Hamisi Dakota hivyo watu wanaotujua sisi
walikuwa wanajua jinsi gani tunavyoishi, Mimi nilishaambiwa hata Dully Skyes
bwana wangu wakati yule ni kaka yangu, ikaenda wakati Nassibu anaanza kutoka
nilikuwa naye karibu katika kumsaidia kazi zake watu wakasema kuwa bwana wangu”
aliongeza Queen Darleen
No comments:
Post a Comment