Mahakama nchini Kenya imewapa madkatari wa wauguzi muda wa
siku tano kumaliza mgomo wao.
Maafisa wa chama cha madaktari walikuwa wamepewa vitisho
kuwa watafungwa ikiwa mgomo huo haungeisha leo.
Madaktari wamekuwa wakiitaka serikali kuheshimu makubaliano
ya mwaka 2013 ya kuwaongezea mishahara.
Wamekataa mshahara walioongezewa na serikali wa asilimia 40
wakisema kuwa ni wa chini kuliko ule walioafikiana mwaka 2013.
Karibu madaktari na wauguzi 5000 kutoka hospitali 2000 za
umma, walianza mgomo wiki ya kwanza ya mwezi Disemba na wagonjwa wamekuwa
wakikosa matibabu.
Jaji katoka mahakama ya ajira amesema kuwa siku hizo tano
sio za mazungumzo bali za kumaliza mgomo.
No comments:
Post a Comment