Bao la Luis Suarez dakika ya mwisho liliokoa jahazi la
Barcelona na kusababisha kutoka sare ya bao moja na Real Betis.
Real Betis ilitawala mechi na mchango wao Dani Ceballos na
Ruben Castro ukazaa matunda wakati Alex Alegria alipoutumbukiza mpira kwenye
wavu.
Awali bao na Barcelona lilikataliwa kutokana kutokuwepo kwa
teknolojia ya kutambua bao likivuka mstari wa goli kwenye michuano ya La Liga.
Hata hivyo Suarez alitumia fursa ya kipekee baada ya kupata
pasi safi kutoka kwa Lionel Messi dakika ya mwisho na kusawazisha .
Barcelona wako pointi moja nyuma ya Real Madrid ambao wana
mechi mbili za kucheza ikiwemo ya nyumbani dhidi ya Real Sociedal siku ya Jumapili
No comments:
Post a Comment