Liverpool wamepanga kumsafirisha kwa ndege ya kibinafsi
mshambuliaji Sadio Mane, kutoka michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa
barani Afrika nchini Gabon, ili kumpa nafasi ya kushiriki mechi na viongozi wa
Ligi Chelsea.
Mane atasafirishwa baada ya Senegal kupoteza tena kwa mabao
5-4 ilipocheza na Cameroon wakai wa mechi za robo fainali siku ya Jumamosi.
Mchezaji huyo wa zamani wa Southampton mwenye umri wa miaka
24, alipoteza penalti muhimu wakati wa mechi hiyo.
Liverpool imeshinda mechi moja tu tangu aondoke kushirika
mechi za kimataifa.
Walishindwa na klabu ya zamani ya Mane kwenye kombe la EFL
siku ya Jumatano na kuondolewa kutoka kombe la FA walipocheza na Wolves.
No comments:
Post a Comment