
RAIS wa Marekani, Donald Trump, ameendelea kuwashambulia
waandishi wa habari, safari hii akiwakejeli kwa ‘kuwaringishia’ barua
aliyoandikiwa na mrithi wake katika Ikulu ya White House, Barack Obama,
akiwaambia licha ya kiu ya habari waliyokuwa nayo, hatafichua ujumbe uliomo
kwenye barua hiyo.
Kwa kawaida nchini Marekani, rais anayeondoka madarakani
humuandikia ujumbe wa barua rais mpya, ujumbe ambao hubeba mambo kadhaa ikiwa
ni pamoja na ushauri unaozingatia uzoefu wa mhusika katika Ikulu ya nchi hiyo.
“Ile nimefika tu ofisini Ikulu nikaikuta barua hii (anaionyesha kwa waandishi) iliyoandikwa kwa umahiri mkubwa kutoka kwa rais Obama,” Trump aliwaeleza waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wake huo, kisha akaongeza; “Ni uungwana wa hali ya juu kwake kuniandikia barua hii, kwa kweli tunaenzi ujumbe wake. Tutaufanyia kazi ujumbe huo na vile vile hatuwezi kufichua ujumbe husika kwenu waandishi wa habari.”
Wakati Obama akiingia madarakani, katika Ikulu ya White
House aliachiwa barua na mtangulizi wake, George W. Bush. Katika barua hiyo,
pamoja na mambo mengine Bush aliandika akimwambia Obama kwamba kutakuwa na
nyakati za “majaribu” ya kiuongozi katika kipindi chake akiwa madarakani. Vile
vile Bush, kupitia ujumbe wa barua hiyo alimuonya Obama kwamba kutaibuka wimbi
la wakosoaji dhidi yake.
“Mungu atakuwa upande wako kwa ajili ya kukupa faraja.
Katika mkondo huo wa faraja, mapenzi ya kifamilia yatakuwa upande wako, nchi
yako haitakutupa, ikiwa ni pamoja nami,” aliandika Bush.
Lakini si tu barua ya Bush kwa Obama ndio iliyowekwa wazi
kwa waandishi wa habari bali pia barua iliyoandikwa na rais Bill Clinton kwa
aliyekuwa mrithi wake Ikulu, rais Bush.
No comments:
Post a Comment